Na Caroline Wambui
ITUGURURU, Kenya, Mei 4 (Thomson Reuters Foundation) – Sehemu kame ya kaunti ya Tharaka Nithi nchini Kenya, haionekani kama yaweza kufanikisha kilimo cha samaki. Lakini mkulima James Muchangi anadhani kuwa samaki ya tilapia na kabare huenda ikawa zao lake la siku za mbeleni kutokana na jinsi ambavyo madiliko ya hali ya hewa inapelekea kuzorota kwa mazao.
Baada ya kufanya utafiti, “niliona kwamba yawezekana kukuza samaki sehemu kame kwa kuwekeza kwa vidimbwi vilivyoinuka na ambavyo havihitaji nafasi kubwa,”alisema mkulima. Sasa anajivunia kukuza samaki 400 katika shamba lake la ekari mbili na nusu.