Kwa sasa, Envl yatenda kazi kama kile kitengo cha usafi na maji ama Sanitation and Water for All (SWA), au kama mashirika za kiraia nchini Sudan. Tunafanya kazi na wadau tofauti, miongoni mwao ni “Sudanese Consumers Protection Society” na “Sudanese Health Promotion Society” kwa kuwa tumejitolea kuendeleza ajenda ya maji na usafi yani Water, Sanitation and Hygiene (WASH) nchini mwetu. Kutenda kazi kwa ushirikiano, ndani ya SWA, imesaidia kupa nguvu sauti zetu na kumulika maswala yetu pamoja na kupatia kipa umbele maswala ya WASH kwa watu wote nchini Sudan.
